Tuesday, 2 February 2016

WAKIMBIZI WANAOJIHUSISHA NA MAPENZI YA JINSIA MOJA WATENGWA.





Ujerumani imefungua kituo cha kwanza cha kuwahifadhi wakimbizi wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wakati ambapo hofu inazidi kuongezeka kuhusu kitisho kinachowakabili watu wa aina hiyo katika makaazi ya kuwahifadhi wakimbizi yaliyofurika.
 
Makaazi hayo mapya ya wakimbizi wenye kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja yapo Nuremberg kusini mwa Ujerumani na yanaweza kuwahifadhi hadi watu wanane kwa mujibu wa Michael Glas ambaye anasimamia shirika linaloitwa Fliederlich lililoanzisha mradi huo.
 
Shirika hilo lilianzisha mpango huo baada ya wakimbizi 20 mashoga kutoa malalamiko kwamba wanahisi kutokuwa salama katika makaazi waliyowekwa.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125