Monday, 1 February 2016

JE WEWE NI MZAZI, AU MZAZI MTARAJIWA? SOMA HII KWA UHAI WA MWANAO USIPUUZE.


Hii ni habari njema kwa wazazi wote wenye watoto wanaosumbuliwa na matatizo ya vichwa kujaa maji au watoto waliozaliwa na matatizo ya mgongo wazi.

 shirika la FOCC Friends of children with cancer wamejitolea kutoa huduma ya upasuaji na uchunguzi kwa watoto wote wenye dalili kama hizo na wale wanaozaliwa na matatizo hayo madaktari wa shirika hili wapo katika hospitali zote za rufaa Tanzania zikiwemo Bugando Mwanza, Rufaa Mbeya, Mhimbili Moi, KCKC Moshi.

Ni wakati sahihi kupunguza matatizo hayo pia wakinamama wanashauriwa kufuata taratibu za lishe bora wakati wa ujauzito ili kuepuka kuzaa watoto wenye vichwa kujaa maji na mgongo wazi. 

Uchunguzi na tiba vitafanyika 04-05 /02/2016 kwa wakaazi wa mbeya Tanzania na nyanda za juu kusini katika hospitali ya rufaa Mbeya.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125