Thursday, 2 April 2015

IDADI YA WANAFUNZI WALIOUWAWA CHUONI KENYA YAFIKIA 147

Miili ya wanafunzi ikiwa imetapakaa darasani.
Serikali ya Kenya imetuma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter ikisema kuwa Watu 500 wameokolewa huku 147 wakiuawa wakiwemo wapiganaji 4 wa kundi la Alshabaab Baadhi ya majeruhi ambao walisafirishwa kwa njia ya ndege kutoka Garissa wamewasili ili kupata matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta mjini Nairobi Kenya.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametuma risala za rambi rambi kwa familia za wale waliouawa katika shambulizi la chuo kikuu cha Garissa kazkazini mashariki mwa Kenya.Kiongozi huyo vilevile amewahakikishia wakenya kwamba serikali yake imechukua hatua za kuwapeleka maafisa wa usalama katika eneo hilo.Amewataka wakenya kuwa watulivu wakatu huu ambapo maafisa wa usalama wanakabiliana na wapiganaji hao.

Waziri wa maswala ya ndani nchini Kenya Joseph Nkaiserry amethibitisha kuwa watu 15 wameuawa huku wengine 53 wakijeruhiwa kufuatia shambulizi la alfajiri katika chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya.miongoni mwa waliokfariki ni walinzi wawili wa mlango wa chuo hicho.Akizungumza kutoka Garissa Nkaiserry amesema kuwa oparesheni ya kuwasaka wahalifu hao itaendelea hadi mateka wote waokolewe.

Serikali ya Kenya imemtaja Mohammed Kuno kama mshukiwa mkuu aliyepanga njama za shambulizi la chuo kikuu mjini Garissa.Katika taarifa kwa vyombo vya habari waziri wa usalama nchini Kenya Joseph Nkaiserry alitoa zawadi ya dola 53,000 kwa mtu yeyote atakayemkamata mshukiwa huyo ama kutoa habari zake.

Kuno anajulikana kama 'Gama'adhere kwa jina maarufu.Mwandishi wa habari wa Kenya Dennis Okari ambaye yuko katika eneo la chuo kikuu cha Garissa ameandika katika mtandao wake wa Twitter akisema kuwa:Wapiganaji hao wako katika jumba la kulala wanafunzi .''ninaweza kusikia milio ya risasi kutoka Kufuatia shambulizi la chuo kikuu cha Garissa ,

Shirika la msalaba mwekundu Red Cross limewataka raia wa Garissa kutoa msaada wa damu.Walioitikia wito huo tayari wameeleka katika hospitali kuu ya Garissa mbapo kituo cha kutoa damu kilianzishwa chini ya mti.Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa Collins Wetangula amesema kuwa wakati wapiganaji hao walipoingia katika nyumba anayolala aliwasikia wakifungua milango na kuwauliza watu iwapo ni waislamu ama wakristo.

''kama wewe ni mkristo unapigwa risasi papo hapo.kila mlio wa risasi nilipousikia nilidhani nitauawa'',aliambia shirika la habari la AP.Amesema kwamba maafisa wa usalama baadaye waliingia kupitia dirisha moja na kumtoa yeye na wenzake hadi katika eneo salama.Maafisa wa matibabu kwa sasa wanaelekea katika hospitali ya kuu ya Garissa nchini Kenya ili kusaidia wale waliojeruhiwa

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125