Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, ametumia ujumbe wake wa Pasaka hapo jana kuwaombea takribani vijana 150 waliouawa kwenye mauaji ya maangamizi katika Chuo Kikuu cha Garissa, kaskazini mashariki mwa Kenya.
Kwenye ujumbe wake huo kwa ulimwengu, Papa ameyasifia pia makubaliano yaliyofikiwa kwenye programu ya nyuklia ya Iran.
Katika ibada hiyo ambayo ilitandwa na mvua kwenye Uwanja wa Mtakarifu Petro, Papa Francis alitoa wito wa kukomeshwa kwa migogoro barani Afrika na kwenye eneo la Mashariki ya Kati, akisema jamii ya kimataifa haipaswi tena kuwachia maafa hayo yanayozalisha wakimbizi wasio idadi.
0 comments:
Post a Comment