Wednesday, 20 May 2015

URUSI YATILIA WASIWASI MAKOMBORA YA MAREKANI YANAYOSIMIKWA UKRAINE. YATOA TAMKO

Urusi imeionya Ukraine dhidi ya uwezekano wa kutegwa mtambo wa Marekani wa kinga ya makombora katika ardhi yake. 

Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Kremlin, ameliambia shirika la habari la nchi hiyo - Interfax, Ukraine ikifanya hivyo, Urusi itachukua hatua zinazolingana na hizo. 

Urusi inauchukulia mpango wa Marekani wa kutega mtambo wa kinga dhidi ya makombora barani Ulaya kuwa ni hatari kwa usalama wake. Kabla ya hapo, Katibu wa Baraza la Usalama la Ukraine, Alexander Turtschinow, alisema mjini Kiev kwamba mtambo kama huo unaweza kuwakinga dhidi ya hujuma kutoka Urusi. 

Rais Petro Poroschenko wa Ukraine alisema katika mahojiano na shirika la utangazaji la Uingereza, BBC, kuwa nchi yake inajiona iko katika vita vya kweli na Urusi. Kiongozi huyo wa Ukraine ameutolea wito Umoja wa Ulaya uendeleze vikwazo dhidi ya serikali ya Urusi.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125