Wednesday, 20 May 2015

ISLAMIC STATE WANASONGA MBELE HUKO SYRIA NA IRAQ WADHIBITI MIJI MUHIMU.


Wanamgambo wa Islamic State wamechukuwa uthibiti wa karibu mji wote wa Palmyra, ulio na kivutuo kikubwa zaidi cha mahame ya kale.

Kuna hofu kwamba wanamgambo hao huenda wakaharibu mahame hayo ambayo shirika la Umoja wa mataifa kuhusu elimu, sayansi na utamaduni, Unesco, limetenga kama eneo la Urathi wa Dunia.

Vikosi vya serikali vimejiondoa katika mji huo baada ya wanamgambo hao kujongea, mmoja wa mashuhuda ameiambia BBC.

Wanamgambo wa IS wamebomoa maeneo kadhaa ya kali ambayo yalitangulia uwepo wa dini ya Kiislamu nchini Iraq ikiwemo miji ya kale ya Hatra na Nimrud.

Awali wanaharakati walisema kundi hilo linathibiti eneo kubwa la kaskazini mwa Tadmur, ambao ni mji wa kisasa ulio mkabala na Palmyra, baada ya kuwashinda wanamgambo walio watiifu kwa rais Bashar al-Assad.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125