Saturday, 6 February 2016

TANZANIA INAWASHIKILIA WATU WATANO KWA MAUAJI YA RUBANI MWINGEREZA. WALINDE TEMBO.



Watu watano wametiwa nguvuni nchini Tanzania kwa tuhuma za kumpiga risasi na kumuua rubani mmoja wa Kiingereza, wakati akiwa kwenye operesheni ya kupambana na ujangili nchini humo.

Shirika la hifadhi ya wanyama la Friedkin la Texas, Marekani, limeripoti kwamba watu wengine zaidi wanatazamiwa kukamatwa kwa mauaji ya rubani huyo, Roger Gower, ambaye aliuawa mwishoni mwa mwezi uliopita karibu na mbuga ya Serengeti.

Miongoni mwa waliokamatwa ni mtu anayetuhumiwa kufyatua bunduki iliyoiangusha helikopta ya Gower, washirika wake, na pia wanachama wa mtandao wa kusambaza silaha haramu.

Shirika la Friedkin linaendesha operesheni ya pamoja ya uhifadhi wa wanyamapori mkoani Maswa, na maeneo mengine nchini Tanzania.

Taifa hilo la Afrika Mashariki linatajwa kuwa kituo kikuu cha ujangili, ambapo idadi ya tembo imeshuka kwa zaidi ya asilimia 60 kutoka mwaka 2009.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125