Marekani, Japan na Korea Kusini zimeitisha kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kujadili hatua ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la roketi hivi leo.
Jaribio hilo la masafa marefu, ambalo Korea Kaskazini imeliita satalaiti yake, linakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya taifa hilo lenye nguvu za kinyuklia, katika rasi ya Korea.
Roketi hilo lilivuuka hadi kupita kisiwa cha Okinawa nchini Japan, ingawa Japan inasema haikuchukuwa hatua ya kulizuwia.
Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, amesema jaribio hilo "halikubaliki", huku Rais Park Guen-Hye wa Korea Kusini, akisema ni "kitendo kisichosameheka", na kulitaka Baraza la Usalama kuchukuwa hatua kali, za kuiadhibu Korea Kaskazini, kwa uchokozi wake huo.
China, rafiki pekee wa Korea Kaskazini, imesema jaribio hilo litaongeza zaidi uhasama kwenye rasi ya Korea, kwa mujibu wa shirika la habari la China, Xinhua.
Jaribio hili linakuja chini ya mwezi mmoja, tangu Korea Kaskazini kufanya jaribio jengine la bomu la atomiki, ambalo hata hivyo wakosoaji wake wanadai halikuwa la kweli.
0 comments:
Post a Comment