Waokoaji kutoka Indonesia wamepata miili watano ya watu waliofariki kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyoikumba wilaya ya Purworejo Ijumaa usiku na bado wanawatafuta watu wengine wawili ambao hawajulikani waliko.
Msemaji wa shirika la taifa la utafutaji na uokoaji,Marsudi,alisema kuwa mvua kubwa ilishababisha maporomoko hayo yaliyotokea saa 20:00 usiku katika mlima ulioko katika kijiji cha Penungkulan.
"Timu ya uokoaji kutoka ofisi ya Java ya kati pamoja na askari, polisi na wafanyakazi wa kujitolea wanawatafuta watu waliopotea,"aliiambia Xinhua kwa njia ya simu.
0 comments:
Post a Comment