Wednesday, 10 February 2016

GARI LA THAMANI KILA MCHEZAJI JE KOMBE LIMELETA FAIDA AU HASARA CONGO?



Wachezaji wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamezawadiwa magari ya kifahari baada ya kushinda Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani (CHAN).


Rais Joseph Kabila amemtunuku kila mchezaji  gari la kifahari la thamani ya $60,000 (£40,000).
Wachezaji hao pia wamepewa nishani.
Chui hao wa Kinshasa walitwaa kombe kwa kulaza Mali 3-0 kwenye fainali na kuwa taifa la kwanza kushinda kombe hilo mara mbili.


anasema mchezaji Heritier Luvumbu Nzinga aliyeumia kwenye michuano hiyo pia ameahidiwa kwamba atasafirishwa ng'ambo kwa matibabu.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125