Mahakama ya juu kabisa nchini Afrika Kusini imesikiliza kesi dhidi ya Rais Jacob Zuma, ambaye anakabiliwa na shutuma za kukiuka katiba.
Vyama vya upinzani vilifungua kesi dhidi ya Zuma, vikimtuhumu kwa rushwa na kutumia mamilioni ya dola katika fedha za umma kuboresha ulinzi kwenye makaazi yake binafsi.
Ukarabati huo ulihusisha bwawa la kuogelea, uga wa kuku na ukumbi wa maonyesho. Baada ya kukana kufanya kosa lolote kwa miezi kadhaa, zuma alisema wiki iliyopita kuwa angerudisha kiasi cha pesa zilizotumika kwenye ukarabati huo.
0 comments:
Post a Comment