Friday, 5 February 2016

BURUNDI HATARI SANA UMOJA WA AFRICA UNAIBEMBELEZA KUPELEKA JESHI LA AMANI.


 
Umoja wa Afrika umewateua viongozi wa mataifa manne wanachama wa Umoja huo ili kujaribu kuishawishi serikali ya Burundi kukubali kuwapokea wanajeshi wa kulinda amani nchini humo. 
 
 Umoja huo wa Afrika wenye makao yake makuu mjini Addis Ababa Ethiopia umewateua Marais Mohammed Ould Abdel Aziz wa Mauritania, Ali Bongo wa Gabon, Macky Sall wa Senegal, Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ambao watakwenda nchini Burundi kuzungumza na Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza juu ya hatua hiyo. 
 
Baraza la usalama na amani la Umoja huo wa Afrika lilitangaza uamuzi wa kuwapeleka wanajeshi 5,000 nchini Burundi kwa kutumia kifungu cha mkataba wa Umoja huo wa Afrika kinachoruhusu kuingilia mambo ya ndani ya nchi mwanachama wa umoja huo hata kama nchi hiyo haikubaliani na hatua hiyo. 
 
Hata hivyo serikali ya Burundi imepinga hatua hiyo ya Umoja wa Afrika na kusema iwapo wanajeshi hao watapekwa nchini humo basi itakichukulia kitendo hicho kama cha uvamizi. 
 
Hadi sasa zaidi ya watu 400 wameuawa nchini Burundi kufuatia machafuko yaliyoibuka baada ya Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania muhula wa tatu wa uongozi.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125