Wanamgambo wa kundi la itikadi kali la Alshabaab wamefanikiwa kuudhibiti mji wa Kusini wa bandari wa Marka nchini Somalia hapo jana saa chache baada ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika na jeshi la serikali ya Somalia kuondoka katika mji huo.
Waasi na mashuhuda wamethibitisha. Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo wanamgambo hao walipandisha bendera yao katika mji huo ulioko kilomita 100 kusini magharibi mwa Mogadishu na kuanza kuwahutubia wakazi wa mji huo kwa kutumia vipaza sauti.
Wanajeshi kadhaa wa Kenya ambao ni sehemu ya wanajeshi wa jeshi la Umoja wa Afrika (AU) nchini Somalia ( AMISOM ) walipoteza maisha wakati wanamgambo hao wa Alshabaab waliposhambulia kambi yao iliyoko eneo la mpakani na Kenya Januari , 15 , mwaka huu hali iliyosababisha vikosi vya Kenya na Somalia kuyatelekeza baadhi ya maeneo.
0 comments:
Post a Comment