Katibu Mkuu wa Umoja wa Maitaifa,Ban Ki-moon,katika ziara yake nchini Burundi alimpongeza Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kwa kukubali kushirikiana na chama cha upinzani katika mazungumzo kwa sababu ya nchi hiyo ambayo imekuwa na migogoro tangu Aprili mwaka jana.
"Jana jioni,nilikutana na watendaji wa kisiasa kutoka chama tawala na chama cha upinzani,na waliahidi kushiriki katika mjadala wa umoja.Pia Rais Nkurunziza alithibitisha kuwa atashiriki katika mazungumzo hayo ya umoja,"Ban alisema baada ya kukutana na Nkurunziza Jumanne (Jana).
Ban alitoa wito kwa viongozi wa kisiasa wa Burundi kufanya mchakato wa kisiasa wa kuaminika ili kuhakikisha wananchi wanaweza kuishi kwa amani na kufurahia haki za binadamu.
0 comments:
Post a Comment