Arsenal jana (Jumanne) walipata kichapo cha kufedhehesha dhidi ya Barcelona pale mabingwa hao wa ligi ya Hispania walipowacharaza mabao 2-0 katika uwanja wa Emirates, ikiwa ni mechi ya kwanza kwenye raundi ya mtoano ya timu 16 ya klabu bingwa barani ulaya (UEFA).
Licha ya ulinzi mkali uliokuwa umewekwa na upande wa Arsenal, Lionel Messi alipata mwanya katika dakika ya 71 na kufungia Barca bao lao la kwanza huku akifunga bao la pili dakika 12 baadaye kupitia mkwaju wa penalti baada ya kuangushwa na Mathieu Flamini.
0 comments:
Post a Comment