Wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon inatarajiwa leo kuuwasilisha mpango wa rais Barack Obama wa kulifunga gereza la Guatanamo. Obama, ambaye aliahidi kulifunga gereza hilo la Marekani nchini Cuba wakati alipoanza awamu ya kwanza madarakani 2009, anajaribu kuitimiza ahadi yake kabla kuondoka ikulu Januari mwakani. Maafisa wa Marekani wamesema mpango huo utataka wafungwa waliochunguzwa na kupitishwa kwa ajili ya uhamisho wapelekwe nchi wanakotokea au katika nchi ya tatu na wengine watakaosalia wapelekwe katika jela za Marekani zenye ulinzi mkali. Wafungwa 91 bado wanazuiliwa katika gereza la Guantanamo, lililofunguliwa mnamo 2012 na rais wa zamani George W. Bush na kuzua ukosoaji kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binaadamu na serikali za mataifa ya kigeni.
Browse » Home
Monday, 22 February 2016
JE OBAMA ATAWEZA KULIFUNGA GEREZA LA GUANTANAMO?
Wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon inatarajiwa leo kuuwasilisha mpango wa rais Barack Obama wa kulifunga gereza la Guatanamo. Obama, ambaye aliahidi kulifunga gereza hilo la Marekani nchini Cuba wakati alipoanza awamu ya kwanza madarakani 2009, anajaribu kuitimiza ahadi yake kabla kuondoka ikulu Januari mwakani. Maafisa wa Marekani wamesema mpango huo utataka wafungwa waliochunguzwa na kupitishwa kwa ajili ya uhamisho wapelekwe nchi wanakotokea au katika nchi ya tatu na wengine watakaosalia wapelekwe katika jela za Marekani zenye ulinzi mkali. Wafungwa 91 bado wanazuiliwa katika gereza la Guantanamo, lililofunguliwa mnamo 2012 na rais wa zamani George W. Bush na kuzua ukosoaji kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binaadamu na serikali za mataifa ya kigeni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment