moja ya nde ge za Iran. |
Iran inasema itanunua ndege 114 za aina ya Airbus ili kufufua ndege zake zilizo kongwe , katika mpango wa kwanza wa kibiashara tangu ilipoondolewa vikwazo vya kiuchumi kufuatia kutekelezwa kwa makubaliano ya mpango wa nyuklia wiki iliyopita.
Waziri wa usafiri wa Iran Abbas Akhoundi amesema mpango huwo utatiwa saini baina ya shirika la usafiri wa anga la Iran na shirika la ndege za aina ya Airbus la Ufaransa wakati wa ziara ya mjini Paris ya rais wa nchi hiyo Hassan Rouhani.
Rais huyo atazuru Ufaransa pamoja na Italia kuanzia LEO Jumatatu hadi Jumatano, ikiwa ni ziara yake ya kwanza barani Ulaya tangu kuanza kutekelezwa kwa mpango wa kupunguza shughuli za kinyuklia na kuondoshewa vikwazo vya kiuchumi.
Rouhani ameyasifu makubaliano hayo yaliyofikiwa baina ya Iran na nchi zenye nguvu duniani, kuwa yameiwezesha nchi hiyo kuanza ukurasa mpya wa kiuchumi huku kwa kurudi tena katika masoko ya ulimwengu.
0 comments:
Post a Comment