Rais wa Burkina faso. |
Vikosi vya jeshi la Burkina Faso vimechapisha taarifa katika vyombo vya habari zinaorodhesha majina na picha za wanajeshi saba wa kikosi cha kumlinda rais wa zamani,
wanaotafutwa kwa kuhusika na uvamizi wa ghala ya silaha karibu na mji mkuu wa Ouagadougou siku mbili zilizopita.
Mamlaka husika zimeshawakamata watu 11 wa kikosi hicho ambacho kinashukiwa kuiba bunduki za aina ya Kalashnikovs pamoja na makombora.
Kikosi hicho cha kumlinda rais wa zamani Blaise Campaore kilivunjwa, baada ya wanajeshi wake kufanya jaribio la mapinduzi yaliyodumu siku sita dhidi ya serikali ya mpito ya nchi hiyo mwezi Septemba,
ambapo mawaziri kadhaa walishikiliwa mateka, kabla ya serikali kurejea tena madarakani kufuatia shinikizo kubwa la kimataifa.
0 comments:
Post a Comment