Theluji kali. |
Hali imeanza kureja taratibu katika miji ya Mashariki nchini Marekani kufuatia kuanguka theluji kubwa kuwahi kutokea katika miongo kadhaa iliyopita.
Kuna taarifa zaidi ya watu ishirini wamefariki kutoka na hali mbaya ya hewa iliyotokana na theluji hiyo.Vituo vya dharura vya kuhudumia wagonjwa vimefunguliwa kuwahudumia watu wanaopata matatizo ya mshutuko wa moyo na kuvunjika mifupa.
Gavana wa jimbo la New York Adrew amewaonya madereva kutoendesha ovyo labda pale kuwepo penye umuhimu.Amesema amri ya kutosafiri iliyotangazwa hapo awali imeondolewa na viwanja vya ndege vimefunguliwa..
Bado kuna hali ambapo magari yanaweza kukwama barabarani. Hivyo tusitafsri vibaya marufuku ya kutosafiri Viwanja vya ndege vimefunguliwa. Na Mamlaka ya viwanja vya ndege imefanya kazi kubwa kusafisha viwanja vya ndege. Na sasa vipo tayari kwa ndege zitakazofanya safari."
Katika mji wa Philadephia mtu mmoja alikuwa akimsaidia jirani yake kuondoa theluji.
Si marekani pekee theluji hiyo imendoka katika nchi nyingine za Asia kama vile Korea kusini, China ,Japan na Hong Kong.
0 comments:
Post a Comment