Saturday, 30 January 2016

MAJESHI YA BANGLADESH, DRC,NIGER, NA SENEGAL YAPATA KASHFA KUU. UN



Umoja wa Mataifa umeweka wazi uraia wa wanajeshi wa kulinda amani wanaoshtumiwa kuwa wamekuwa wakiwadhulumu watoto kingono Jamhuri ya Afrika ya kati.

Washukiwa hao ni raia wa Bangladesh, the DRC, Niger na Senegal.

Akihutubia wanahabari mjini New York, afisa mkuu wa UN Anthony Banbury karibu atokwe na machozi wakati alipotangaza kesi za hivi karibuni za unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto.

Mwezi ulopita, jopo huru lilikashifu jibu la UN kuhusu madai hayo kama yenye makosa makubwa.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125