Saturday, 30 January 2016

HODI BURUNDI JESHI LA AFRICA LAWEZA KUTUA MUDA WOWOTE



Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bakn Ki-moon jana ameupongeza mpango wa Umoja wa Afrika wa kutayarisha ujumbe utakaokuwa na kazi ya kuzuia na kulinda ghasia za kikabila na kisiasa nchini Burundi. Umoja wa Afrika unategemea kulipigia kura pendekezo hilo la kutuma wanajeshi 5,000 nchini humo. 
 
wakati huo huo, rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameahidi kupambana na wanajeshi hao wa kulinda amani watakaotumwa na Umoja wa Afrika. 
 
Kulingana na Umoja wa Mataifa, zaidi ya Warundi 400 wameuawa tangu kuzuka kwa machafuko mwezi Aprili mwaka jana yanayotokana na hatua ya rais Nkurunziza ya kuingia madarakani kwa muhula wa tatu huku upinzani ukisema ni ukiukwaji wa katiba. Halikadhalika makundi mbalimbali yanayomiliki silaha yamekuwa yakifanya mashambulizi nchini humo yakipambana na ukandamizaji wa polisi.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125