Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan jana ameishutuma Urusi kwa kuchukua hatua alizosema zimekosa uwajibikaji, na ambazo zinatishia amani ya dunia.
Matamshi hayo ya Erdogan yalikuja masaa kadhaa baada ya Uturuki kutangaza kwamba ndege ya Kirusi iliingia katika anga zake kinyume na sheria, licha ya kitengo cha kulinda anga kuionya ndege hiyo mara kadhaa kwa Kirusi na kwa Kiiengereza.
Msemaji mkuu wa wizara ya usalama ya Urusi Igor Konashenkov aliyajibu madai hayo leo hii, na kukana kwamba hakuna ukiukwaji wa sheria uliofanywa na Urusi ndani ya anga ya Uturuki. Wakati huo huo, mkuu wa jumuiya ya kujihami ya NATO ameitaka Urusi kuheshimu kikamilifu anga ya Uturuki.
0 comments:
Post a Comment