Friday, 29 January 2016

UHOLANZI YAJIUNGA RASMI NA VITA HUKO SYRIA NA IRAQ.




Uholanzi imeamua kujiunga na mashambulizi yanayoongozwa na Marekani dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic State (ISIS) nchini Iraq na Syria.

"Tukiweza kuyamaliza maficho ya kikundi hiki yaliyoko Iraq na Syria pia tutaweza kuzuia mashambulizi," Waziri Mkuu Mark Rutte kutoka Uholanzi alisema katika mkutano wa waandishi wa habari.

Baraza la mawaziri wa Uholanzi pia wamekubali hatua ambazo zitatumiwa kutatua migogoro huko Iraq na Syria kwa njia ya kisiasa na kibinadamu.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125