Vikosi vya jeshi la Marekani na Ukraine vimeanza rasmi luteka ya pamoja yenye lengo la kuisaidia nchi hiyo kuimarisha ulinzi wake dhidi ya mashambulizi kutoka kwa wapiganaji wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Urusi mashariki mwa Ukraine.
Akizungumza katika kituo cha kijeshi katika jimbo la magharibi la Lviv, rais wa Ukraine Petro Poroshenko amesema majeshi ya ulinzi yanahitaji kujengwa upya kuweza kuzuwia vitisho vya kijeshi vya kimataifa.
Mazowezi hayo ya kijeshi yamesababisha Urusi kuonesha hali ya kutoridhika, na kuyaeleza kuwa ni sababu muhimu ya kutokuwa na usalama katika eneo hilo.
Wanajeshi 300 wa Marekani wanaohusika katika luteka hiyo wamekwenda Ukraine wiki iliyopita na watafanyakazi pamoja na wanajeshi 900 wa jeshi la taifa la Ukraine.
0 comments:
Post a Comment