Thursday, 16 April 2015

BRIGEDIA JENERALI WA JESHI LA TANZANIA (JWTZ) ATEULIWA KUWA MKUU WA UMOJA WA AFRICA (AU) NCHINI SUDAN YA KUSINI

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Dr. Nkosanzana Dlamini Zuma, 

amemteua, Brigedia Jenerali Sara Thomas Rwambali kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( 

JWTZ),kuwa Mwakilishi Maalum na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Afrika Sudan ya Kusini .

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na AU na nakala yake 

kutumwa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, inaeleza kwamba 

makazi ya Brigedia Jenerali Sara Thomas Rwambali yatakuwa Juba.

Pamoja na uteuzi wa Brigedia Jenerali Sara Rwambali, Dr. Nkosazana Dlamini Zuma 

pia amewateua Madame Josephine- Charlotte Mayuma Kala kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya 

Kongo, anayekuwa Mwakilishi Maalum na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Afrika huko Cote 

d’Ivoire na makazi yake yakiwa Abidjan.

Wengine walioteuliwa ni Madame Nyiramatama kutoka Rwanda, anayekuwa Mkuu 

wa Ofisi ya AU huko Chad , makazi yake yakiwa Ndjamena na Dr. Arvin Boolel kutoka 

Mauritius anayekuwa Mwakilishi Maalum na Mkuu wa Ofisi ya AU katika Maziwa Makuu 

Burundi na makazi yake yakiwa Bujumbura.

Taarifa kwa vyombo vya Habari kutoka AU inaeleza zaidi kwamba uteuzi huo ni sehemu 

ya AU ya kuhakikisha uwepo wake katika kila eneo na vile vile kuunga mkono juhudi 

zinazolenga katika kukuza Amani na Usalama Barani Afrika

“Ninatoa pongezi zake za dhati kwa wateuliwa ambao ni viongozi wa ngazi za juu na 

wenye sifa za kutukuka katika utumishi wa umma wakiwa na uzoefu mkubwa katika eneo la 

amani na usalama. Si jambo la ajabu kwamba wateule watatu kati ya wanne ni wanawake” 

anasema Dr. Zuma

Na kuongeza, “katika mwaka huu wa 2015, ambao Umoja wa Afrika umejikita katika 

uwezeshwaji wa wanawake. Ninayo matumaini makubwa kwamba AU na Afrika kwa ujumla 

itanufaika na utaalamu na uzoefu mkubwa na uwezo wa kiuongozi kutoka kwa wateuliwa 

hawa”.

Mwenyekiti wa Kamishna ya AU pia ametoa wito kwa wadau wote kuwapatia 

ushirikiano wateuliwa hao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ukamilifu kwa maslahi ya 

Bara la Afrika, huku akitoa shukrani kwa wawakilishi ambao wanamaliza muda wao.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125