Mfalme wa Wazulu Goodwill Zwelithini amekana kuanzisha chuki dhidi ya wageni nchini Afrika kusini baada ya kushutumiwa kuzusha ghasia hizo ambazo zimesababisha watu saba kuuwawa na kuwalazimisha maelfu wengine kuyahama majumba yao.
Zwelithini mwezi uliopita alitoa hotuba yenye jazba akiwalaumu wahamiaji kutokana na kuongezeka kwa uhalifu na kusema wanapaswa kuondoka nchini humo, katika hotuba ambayo inaonekana kushawishi wimbi la mashambulizi dhidi ya Wazimbabwe, Wasomali, Wamalawi na wageni wengine.
Lakini ameuambia mkutano wa kikabila uliohudhuriwa na maelfu ya Wazulu katika mji wa bandari wa Durban kwamba amenukuliwa vibaya.
Ameongeza kuwa ghasia hizi zilizoelekezwa kwa kaka zetu na dada zetu ni fedheha kubwa. Hotuba yake amesema ilielekezwa kwa polisi , ikitoa wito wa kuchukua hatua kali za ulinzi, lakini hilo halikuripotiwa.
Maafisa nchini Afrika kusini wamepata shida kuzuwia makundi katika mji wa kibiashara wa Johannesburg na Durban wakiwasaka wahamiaji.
0 comments:
Post a Comment