Rais Xi Jinping wa China jana huko Islamabad kwa nyakati tofauti alikutana na rais Mamnoon Hussain wa Pakistan, viongozi wa vyama mbalimbali vya nchi hiyo na kutoa tuzo ya urafiki kwa watu binafsi na mashirika ya Pakistan yaliyotoa michango katika kuenzi urafiki kati ya nchi hizo mbili.
Alipofanya mazungumzo na rais Hussain, rais Xi ametoa mapendekezo matano kuhusu kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili, yaani kudumisha mawasiliano ya ngazi ya juu, kufanya ushirikiano wa kunufaishana na kutimiza maendeleo kwa pamoja kwa kutoa kipaumbele katika ujenzi wa ushoroba wa kiuchumi kati ya China na Pakistan, kuimarisha ushirikiano wa kiusalama, kufanikisha shughuli za mwaka wa nchi katika kila upande, na kuimarisha uratibu na ushirikiano katika masuala muhimu ya kimataifa yakiwemo mageuzi ya Umoja wa Mataifa, usalama wa nishati na chakula.
Alipokutana na viongozi wa vyama vya siasa, rais Xi alisisitiza kuwa Pakistan ni rafiki wa chanda na pete kwa China, na chama cha kikomunisti cha China kinatilia maanani kuhimiza uhusiano na vyama mbalimbali vya Pakistan na kuongeza mawasiliano na ushirikiano kati ya vyama.
0 comments:
Post a Comment