Uingereza na Ufaransa zimekubali hapo jana kutafuta idhini ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya operesheni ya kijeshi ya Umoja wa Ulaya dhidi ya watu wanaosafirisha binaadamu kwa magendo katika juhudi za kuzuwiya idadi inayongezeka ya wahamiaji wanaokufa wakati wakikimbilia Ulaya kutafuta maisha bora.
Katika mkutano wa dharura mjini Brussels hapo jana viongozi wa Umoja wa Ulaya pia wameamuwa kuongeza mara tatu zaidi kiwango cha fedha kwa ajili ya operesheni ya kuwatafuta na kuwaokowa wahamiaji inayoendeshwa na umoja huo wakati habari za kutisha za vifo vya wahamiaji zikizidi kuibuka ambapo wiki iliopita zaidi ya wakimbizi 900 wamepoteza maisha yao katika bahari ya Mediterenia.Rais wa Umoja wa Ulaya Donald Tusk amesema mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini amepewa jukumu la kupendekeza hatua ya kuteka na kuharibu mashua za watu wanaowasafirisha binaadamu kwa magendo kabla ya vyombo hivyo kuanza kutumika.
Hata hivyo viongozi hao wameshindwa kukubaliana juu ya suala nyeti la namna ya kuwashughulikia wahamiaji ambao wengi wao huondokea Libya nchi iliokumbwa na machafuko.
0 comments:
Post a Comment