Mkutano mkubwa wa kimataifa unaowaleta pamoja mawaziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani na Cuba, unafanyika leo Ijumaa nchini Panama.
Ni mkutano mkubwa na wenye hadhi ya juu zaidi kati ya mataifa hayo mawili ambayo hayajakuwa na na uhusiano mwema tangu uhuru wa Cuba zaidi ya nusu karne iliyopita.
Waziri wa masuala ya nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Cuba,Bruno Rodriguez wametumia muda wa saa mbili katika mkutano wa faragha unaoelezwa na Marekani kama wenye manufaa makubwa.
Wakati mkutano huo ukiendelea Rais Barrack Obama na mwenzake wa Cuba Raul Castro pia wanatarajiwa kukutana kwa mara ya kwanza.
Hapo jana seneta mmoja mashuhuri nchini Marekani Ben Cardin alipendekeza kuiondoa jina la Cuba kutoka katika orodha ya mataifa yanayofadhili ugaidi duniani.Hata hivyo Marekani imesema kuwa iko tayari kubadili msimamo wake dhidi ya Cuba.
Iwapo Cuba itaondolewa katika orodha hiyo, bila shaka hilo litatoa mwanya kwa mataifa hayo mawili kufungua ubalozi.
Hadi kufikia sasa taarifa kamili kuhusu walichojadili wawili hao haijabainika.
Mkutano sawia na huu uliwahi fanyika mara ya mwisho mwaka wa 1959 Fidel Castro alipokutana na aliyekuwa makamu wa rais wa Mareakani wakati huo Richard Nixon.
Japo mahusiano yalikatika miaka miwli baadaye rais Obama alitangaza wazi kuwa mambo yamebadilika na kuwa Marekani sasa itafungua ukurasa mpya wa uhusiano baina ya nchi yake na Cuba.
0 comments:
Post a Comment