Kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC, iliyoko the Hague Uholanzi, Fatou Bensouda, amesema kuwa kundi la wapiganaji la Islamic State,
limetekeleza uhalifu wa hali na ukatili mkubwa nchini Syria na Iraq.
Bensouda amesema uhalifu huo unahatarisha amani, usalama sio wa eneo hilo tu bali dunia kwa ujumla, lakini amekariri kuwa Iraq na Syria sio wanachama wa mahakama hiyo.Wengi wa wapiganaji wa kundi hilo ni raia wa Kigeni ndio maana mwendesha mashtaka huyo mkuu anasema hana budi ila kusalimu amri.
Maelfu ya wapiganaji wa kigeni wamejiunga na wapiganaji wa ISIS, wakiwemo raia wa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Ubelgiji, Australia na Tunisia.
Licha ya kuwa nchi hizi ni wanachama wa mahakama ya ICC, Bensouda anasema kuwa kundi hilo la ISIS linaongozwa na raia wa Iraq na Syria.
Na kwa sababu nchi hizo sio wanachama wa ICC, Bi Bensouda amesema kuwa uwezekano wa kuchunguza wale waliohusika zaidi chini ya uongoza wa ICC ni finyu kabisa.
Aidha ametoa wito kwa mataifa wanachama kutafuta mbinu za kuwawajibisha wale waliohusika.
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa halina mamlaka kuwasilisha kesi katika mahakama hiyo kuhusiana na hali ilivyo nchini Iraq na Syria.
Ameongeza kuwa kuwa uhalifu unaondelea kutekelezwa nchi humo unakiuka maadili yote ya kibinadam na ni sharti waliohusika kufunguliwa mashtaka.
0 comments:
Post a Comment