Saturday, 11 April 2015

UGAID WASABABISHA KENYA KUIFUNGA KAMBI YA WAKIMBIZI YA DADAAB NDIO KAMBI KUBWA ZAIDI DUNIANI.


Serikali ya Kenya imeupatia Umoja wa Mataifa makataa ya miezi mitatu kuwahamisha wakimbizi wa Somalia wapatao nusu milioni hadi nchini Somalia.

Naibu rais William Ruto amesema kuwa iwapo Umoja wa mataifa utakataa kuwahamisha wakimbizi hao, Kenya itachukua jukumu la kuwandoa.

Makataa hayo yanajiri siku kadhaa baada ya shambulizi la chuo kikuu cha Garissa ambapo takriban watu 148 waliuawa na kundi la wapiganaji wa Al-shaabab.

Baadhi ya wakimbizi wamekuwa wakiishi katika kambi za Dadaab mashariki ya taifa hilo kwa zaidi ya miongo miwili.

Kenya imelishtumu kundi la Alshabaab kwa kujificha katika kambi hizo huku likiwasajili wanachama wapya.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125