Wednesday, 25 March 2015

UHUSIANO BAINA YA MAREKANI NA ISRAEL WAZOROTA KWA KIWANGO CHA JUU HIVI SASA.



Picha ya rais Obama na Netanyahu katika kikao maalumu.

Rais Barack Obama wa Marekani amesisitiza msimamo wa serikali kuelekea suluhisho la mataifa mawili huru ya Israel na Palestina, huku uhusiano kati ya nchi yake na Israel umefikia tena katika kiwango cha chini kabisa.

Akizungumza mjini Washington hapo jana, Obama ambaye serikali yake imemshutumu Netanyahu kuchochea ubaguzi kwenye kampeni zake za kuchaguliwa tena kuwa waziri mkuu katikati ya mwezi huu, alisema ingawa Netanyahu anawakilisha maslahi ya nchi yake kadiri anavyoona inafaa, ndivyo pia anavyofanya yeye Obama:

Waziri mkuu Benjamin Netanyahu aliyechaguliwa tena hivi karibuni amekosoa mazungumzo ya kimataifa na Iran kuhusiana na mpango wake wa kinyuklia, na kusema wazi kuwa taifa la Palestina halitaundwa katika wakati wake akiwa waziri mkuu.

Pia jana, Rais Obama alikutana na rais wa Afghanistan Ashraf Ghani na kukubaliana kupunguza kasi ya kuyaondoa majeshi ya Marekani kutoka nchi hiyo. Obama amekubali kubakisha wanajeshi 10,000 nchini Afghanistan hadi mwishoni mwa mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125