![]() |
| Picha hii ya kundi la tembo ilipigwa katika mbuga ya masai mara nchini Kenya. |
Wataalamu wanakutana nchini Botswana katika mkutano wa kutafuta njia za kukomesha biashara haramu ya wanyama pori ambayo inapunguza idadi ya tembo, faru na wanyama wengine ambao wako katika hatari ya kutoweka.
Wakionya juu ya mzozo mkubwa wa kupotea kwa wanyama pori, wataalamu watashinikiza kutekelezwa kwa ahadi zilizotolewa na mataifa 46 katika mkutano mwaka jana mjini London kuhusu biashara ya wanyama pori, hatua iliyosifiwa kuwa ni muhimu katika mapambano ya kuwalinda wanyama walio katika hatari ya kutoweka.
Tembo, faru na chui ni miongoni mwa wanyama wanaowindwa na majangili pamoja na wasafirishaji haramu wa wanyama hao. Lakini wanyama wengine pia kama kasa na kakakuona, pamoja na mimea isiyokuwa ya kawaida inaathirika.





0 comments:
Post a Comment