Tuesday, 24 March 2015

NDEGE YA ABIRIA YA SHIRIKA LA GERMANWINGS AIRBUS A320 IMEANGUKA HUKO UFARANSA IKIWA NA WATU 148.

Ndege ilioayoangu  ni kama hii.


Ndege ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320 Imeanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa.

Ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 142 na wahudumu 6 ikitoka Barcelona Uhispania kuelekea Duesseldorf.

Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa chini ya nembo Germanwings imeripotiwa kuanguka karibu na mji wa Digne.

Ndege hiyo ya A320 ilianguka saa tano asubuhi katika Kusini mwa Milima ya Alps.

Viongozi wa Ujerumani na Ufaransa wanaendelea kushauriana kuhusiana na mkasa huo unaowakabilia macho.

Ndege hiyo ya Ujerumani ilianguka katika eneo lisilo na mijengo ambalo halifikiki kwa urahisi nchini Ufaransa Kusini mwa Milima ya Alps.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125