Tuesday, 24 March 2015

MAREKANI INAWEZA KUIPA UKRAINE SILAHA NZITO ILI KUPAMBANA NA WAASI WANAOUNGWA MKONO NA URUSI


Rais wa Marekani Barack Obama akisisitiza jambo katika ikulu ya Marekani.

Baraza la Wawakilishi la Marekani limeunga mkono azimio linalomtaka rais wa nchi hiyo Barack Obama kuipatia silaha Ukraine ili iweze kujilinda dhid ya waasi wanaoungwa mkono na Urusi. 

Wawakilishi 348 walipiga kura kulikubali azimio hilo, huku 48 tu wakipiga kura zao kulipinga.

Wabunge wa vyama vyote katika bunge la Marekani wanaunga mkono hatua ya kuisaidia kijeshi Ukraine katika vita vyake dhidi ya waasi wa Mashariki.

Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani wamesema serikali ya rais Obama inatafakari uwezekano wa kuipatia silaha Ukraine, huku wakisubiri kuona namna makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwezi Februari yanavyotekelezwa.

Rais wa Urusi Vladimir Putin anakanusha tuhuma kwamba nchi yake inawasaidia waasi wa Mashariki mwa Ukraine wanaotaka kujitenga.



0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125