Monday, 23 March 2015

MAUAJI YA ALBINO TANZANIA JESHI LA POLISI LAWASAKA WAGANGA WA JADI KWA UDI NA UVUMBA.


Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya akionyesha vifaa vya waganga wa jadi vinavyotumika kupiga ramli.

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya nchini Tanzania limewakamata watu 15 na kuwafikisha Mahakamani wakituhumiwa kujihusisha na upigaji wa ramli chonganishi ikiwa ni hatua ya kuwasaka waganga wasiokuwa na vibali katika kukomesha maovu yanayotokana na imani za kishirikina.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi amezungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema kesi hizo zipo kwenye hatua mbali mbali.

Amesema kuwa katika msako ambao ulianza tangu Machi 6, mwaka huu, Tayari Jeshi hilo limewakamata waganga wa jadi 23 wanaojihusisha na upigaji waramli hizo chonganishi.

ameongeza kuwa watuhumiwa 15 walifikishwa mahakamani na kesi zao zipo katika hatua tofauti na kwamba watuhumiwa sita upelelezi bado unaendelea na mtuhumiwa mmoja taratibu zinafanywa ili aweze kufikishwa mahakamani.

Amesema watuhumiwa walikamatwa katika wilaya tofauti na idadi yao kwenye mabano ambazi ni Wilaya ya Mbeya (7), Chunya(12) , momba(2),Mbozi (01) pamoja na Kyela(01).Aidha Msangi alisema baadhi ya zana ambazo wamekamatwa nazo waganga hao ni pamoja na nyara vza serikali na zana zisizokuwa na nyara zisizokuwa za serikali .

Hata hivyo Kamanda Msangi alitoa wito kwa wananchi kujiepusha na tabia za kusadiki imani za ushirikina kwa kupiga ramli ili kutatua matatizo yao kwenye jamii.Pia alitoa onyo kwa wananchi wanaoshirikiana kuwaficha waganga wa kienyeji wanaojihusisha na upigaji wa ramli chonganishi ambazo zinadaiwa kuwa chanzo cha uhalifu unaohusiana na imani za kishirikina.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125