Siku moja baada ya kuwapokea masheikh 50 kutoka Bagamoyo, mbunge wa monduli Edward Lowasa amepokea makundi ya wanafunzi wa vyuo vikuu,
madereva wa pikipiki (bodaboda) na wamachinga wa Dodoma wakimtaka achukue fomu
kuwania nafasi hiyo.
Tayari mbunge huyo alishampokea Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM, Dk Rapahel Chegeni na baadaye kundi marafiki wa Lowassa kutoka
mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
Wanafunzi hao ambao waliongozana na baadhi ya wahadhiri wao walitoka
Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), St John, Mipango na Chuo cha Biashara (CBE), Tawi
la Dodoma.
0 comments:
Post a Comment