Monday, 23 March 2015

MAAFISA KADHAA WA JESHI LA SYRIA WATEKWA NYARA NA WAASI BAADA YA HELIKOPTA YAO KUANGUKA.

Waasi wa Syria wamewateka nyara maafisa kadhaa wa kijeshi wa serikali baada ya helikopta waliyokuwa wakisafiria kuanguka katika mji unaoshikiliwa na waasi wa kaskazini magharibi mwa Syria.

Kituo cha habari cha Idlib na shirika la Syria la kufatilia haki za binaadamu, wamesema helikopta hiyo ilianguka jana karibu na mji wa Jabal al-Zawiya kwenye jimbo la Idlib.

Mkurugenzi wa shirika hilo, Rami Abdurahman, amesema waasi hao, likiwemo kundi la al Nusra Front, linalofungamana na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda, wanawashikilia mateka wafanyakazi wanne wa helikopta hiyo.


Imeripotiwa kuwa askari mmoja alinusurika katika ajali hiyo, lakini aliuawa na waasi hao na askari mwingine wa sita hajulikani aliko.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125