Monday, 23 March 2015

MUASISI WA TAIFA LA SINGAPORE AFARIKI DUNIA NA UMRI WA MIAKA 91



Waombolezaji wakionyesha hisia na heshima zao sehemu maalumu ya maombolezo.
Kiongozi mashuhuri wa Singapore, anayejulikama kama baba wa taifa hilo , Lee Kuan Yew amefariki. 

Serikali ya nchi hiyo imetangaza hii leo kwamba Lee mwenye umri wa miaka 91 alilazwa hospitalini mapema Februari akiwa anaugua ugonjwa wa kichomi, na amekuwa akipumua kwa kutumia mashine katika kitengo cha wagonjwa mahututi tangu wakati huo.

Mtoto wa Lee , Lee Hsien Loong ambaye ni waziri mkuu ametangaza muda wa maombolezo kitaifa kuanzia leo Jumatatu hadi Machi 29.


Rais wa Marekani Barack Obama ametuma salamu zake za rambi rambi na kumuelezea Lee kuwa mtu aliyeona mbali. 

Nae katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amesikitishwa mno na kifo cha Lee , na kusema alikuwa mtu muhimu katika bara la Asia.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125