Monday, 23 March 2015

BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LAMUUNGA MKONO RAIS WA YEMEN


Askari wa kulinda amani wa umoja wa mataifa wakiwa doria huko Sudan ya kusini ;Darfu


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetangaza kwa kauli moja kumuunga mkono Rais wa Yemen, Abed Rabbo Mansour Hadi. 

Baraza hilo pia linaunga mkono suala la kuwepo umoja na mshikamano wa Yemen, huku kukiwa na onyo kwamba nchi hiyo inaelekea kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. 

Akizungumza katika mji wa kusini wa Aden, ambao ameutangaza kuwa mji mkuu wa muda, Rais Hadi amewataka wanamgambo wa Kishia-Houthi, kuondoka kwenye mji mkuu wa Sanaa. 

Wakati huo huo, waasi wa Houthi wametangaza upya hatua yao ya kuitwaa miji yote ya Yemen. 

Hatua hiyo inatokana na mashambulizi ya kujitoa muhanga katika misikiti mjini Sanaa ambapo watu 137 waliuwawa. 

Hapo jana, waasi wa Houthi waliuteka mji wa Taiz, ambao ni wa tatu kwa ukubwa nchini Yemen.


0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125