Wednesday, 2 March 2016

DR SLAA AFUNGA NDOA KWA MBWEMBWE TAZAMA PICHA.



Hatimaye aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa amekamilisha ndoto yake kubwa baada ya jana kufunga ndoa na mpenzi wake, Josephine Mushumbusi nchini Canada. Ingawa Dk. Slaa aliwahi kuwa Padri wa Kanisa Katoliki, wawili hao wanadaiwa kufunga ndoa kwenye kanisa tofauti la Kikristo ingawa jina la kanisa hilo halikufahamika mara moja. Jaribio la kufunga ndoa kwa wawili hao tangu mwaka 2010 lilikumbwa na vizingiti ikiwa ni pamoja na mume wa zamani wa Josephine kufungua kesi mahakamani akidai kuwa bado mwanamke huyo ni mkewe halali.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125