Sunday, 28 February 2016

JAMBAZI LILIOONGOZA MAUAJI NA UPORAJI BENKI YA ACCESS MBAGALA LAKAMATWA.



Kiongozi wa majambazi yaliovamia Benki ya Access tawi la Mbagala jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kuwaua watu sita na kabla ya kupora kitita cha shilingi milioni 20, anadaiwa kutiwa mbaroni na kikosi maalum cha Jeshi la Polisi kinachowahusisha pia wanajeshi. Vyanzo vya kuaminika vimeeleza kuwa kiongozi huyo wa majambazi 12 waliotekeleza tukio hilo alikamatwa jana majira ya saa tano asubuhi katika eneo la Sinza Mori jijini Dar es Salaam, baada ya kutajwa na majambazi wenzake waliokamatwa siku chache zilizopita.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © 2025 Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125