Monday, 15 February 2016

TAZAMA KOMBORA LA KISASA LA MAREKANI LILITUMWA KIMAKOSA CUBA, NI HATARI



Cuba imerudisha kombora la Marekani aina ya Hellfire ambalo lilipelekwa mjini Havana kimakosa kutoka bara Uropa mwaka wa 2014.

Kombora hilo linanoelekezwa na teknolojia ya laser lilifika mjini Havana Julai mwaka wa 2014 kutoka Paris, wizara ya mambo ya nje ya Cuba imesema. "Ilitutia hofu kuona kombora lililotengenezwa Marekani hapa bila stakabadhi za kuidhinisha kuingizwa kwake humu nchini," taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ilisema.

Cuba ilianzisha mpango wa kurudishia Marekani kombora hilo baada ya maafisa wa serikali ya Marekani kutoa maelezo kulihusu na kutoa ombi kwamba lirudishwe. 
 
Maafisa wa ulinzi wa Marekani walisafiri hadi Havana siku ya Jimamosi na kulisafirisha hilo kombora hadi Marekani.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125