Kuelekea uchaguzi mkuu wa Uganda unaotarajiwa kufanyika Alhamis ya wiki hii, leo polisi wa Uganda wameshikilia mgombea urais kupitia chama cha FDC wakati akijaribu kufanya kampeni kwenye kitovu cha mji wa Kampala ambako polisi walizuia.
Polisi walifyatua mabomu kadhaa ya machozi kwenye barabara ya Kampala-Jinja ili kutawanya wafuasi wa Kiza Besigye kisha kumuingiza ndani ya gari ya polisi na kumpeleka kituoni huku wafuasi wake wakimfata kwa usafiri wa pikipiki.
Besigye tayari ameshapoteza chaguzi tatu ambazo zilikumbwa na utata dhidi ya Rais wa sasa, Yoweri Museveni ambae yuko madarakani kwa miaka 30 sasa na Besigye alishawahi kuwa daktari wake wakati yuko msituni hadi alipoamua kuwa mwanasiasa na kumuita Museveni kuwa dikteta.
0 comments:
Post a Comment