Sunday, 28 February 2016

TALIBAN WASALIMU AMRI KWA SERIKALI



Takriban wapiganaji 130 wa kundi la Taliban wamesalimu amri kwa serikali katika mkoa wa Faryab, kaskazini mwa Afghanistan, gavana wa mkoa huo amesema.

"Tunawakaribisha ndugu zetu 130 ambao wamejitenga na vurugu na kujiunga na juhudi zetu za kuleta amani na maridhiano," Sayyed Anwar Saadat, gavana wa Faryab alisema. Saadat alisema kuwa serikali itafanya juhudi zote kuwaunganisha watu hao waliokuwa wapiganaji na familia zao.

Wapiganaji hao pia walikabidhi serikali shehena ya silaha aina mbali mbali pamoja na risasi. Zaidi ya wapiganaji 10,000 wamesalimu amri kwa serikali ya Afghanistan katika kipindi cha miaka 6 zilizopita na kujiunga na kampeni ya amani na maridhiano inayoongozwa na serikali hiyo. Upande wa Taliban haujatoa taarifa kuhusu hatua ya wanachama hao 130 kusalimu amri.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125