Friday, 26 February 2016

HUYU NDIYE RAIS MPYA WA FIFA HONGERA.


MSWISI mwenye asili ya Italia, Gianni Infantino amekuwa Rais wa tisa wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika mjini Zurich, Uswisi leo na akaahidi kurejesha hadhi ya soka uliwenguni katika zama mpya.
 
Kura za uchaguzi wa FIFA jana zimepigwa mara mbili kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 42 baada ya Infantino, Katibu wa zamani wa UEFA kutomshinda kwa nusu ya kura mpinzani wake wa karibu, Sheik Salman bin Ibrahim al Khalifa wa Bahrain katika Raundi ya kwanza.
 
Katika kura za raundi ya pili zilizohusisha wapinzani hao wawili tu, Infantino alikusanya 115 huku Sheik Salman, akipata 88 na kuwa Mswisi wa pili mfululizo kukamata Urais wa FIFA, baada ya Sepp Blatter.
Mwanasjeria huyo kitaaluma mwenye umri wa miaka 45 anatokea Brig mjini Valais, Uswisi, kiasi cha maili sita kutoka nyumbani kwao Blatter, Visp.
 
Blatter alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1998 na akaendelea kushinda chaguzi tano zilizofuata, ukiwemo wa Mei mwaka jana, lakini akalazimika kujiuzulu siku kadhaa baadaye kufuatia tuhuma na ukosefu wa maadili zilizoambatana na kufungiwa miaka sita kujihusisha na masuala ya soka, ambayo ameendelea kujihusisha nayo.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125