Friday, 5 February 2016

SAUDI ARABIA KUTUMA JESHI LA NCHI KAVU SYRIA KUPAMBANA ANA KWA NA KUNDI LA IS.



Saudi Arabia inakusudia kupeleka wanajeshi wake wa aridhini nchini Syria kwa ajili ya kupambana dhidi ya wanamgambo wa kundi la itikadi kali la Dola la Kiisilamu iwapo washirika wake katika mapambano hayo watakubaliana na hoja hiyo katika kikao kilicho pangwa kufanyika mjini Brussels. 
 
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Saudi Arabia Brigedia Jenerali Ahmed Asiri , Saudi Arabia imekuwa ikishirikiana na washirika wake katika mapambano dhidi ya kundi hilo la Dola la Kiisilamu tangu operesheni ya mashambulizi ya anga inayoongozwa na Marekani dhidi ya kundi hilo ilipoanza Septemba 2014 na kuwa sasa iko tayari kutoa wanajeshi wake wa ardhini.
 
 Marekani inaratibu kikao kitakachowahusisha mawaziri wa ulinzi kutoka mataifa yanayoshiriki katika mapambano dhidi ya kundi hilo la dola la kiisilamu kitakachofanyika mjini Brussels mwezi huu. Kwa sasa Saudi Arabia inashiriki pia katika mapambano dhidi ya waasi nchini Yemen.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125