Miaka saba ndani ya utawala wake , rais Barack Obama anafanya ziara yake ya kwanza katika msikiti nchini Marekani leo, akitoa ishara ya kupinga matamshi makali ya wagombea wa chama cha Republican dhidi ya Waisilamu.
Obama ambaye babu yake alibadili dini na kuwa Muislamu , atafanya ziara hiyo fupi katika msikiti mjini Baltimore , ambako atakutana na viongozi wa jamii ya Waislamu na kutoa hotuba fupi.
Aliwahi kutembelea misikiti nchini Malaysia , Indonesia na Misri akiwa rais, lakini bado hajawahi kutembelea msikiti nchini Marekani.
Sera za mambo ya kigeni za Obama zimelenga katika kuimarisha mahusiano na mataifa ya Kiislamu, kuanzia kufikia makubaliano na Iran na kuwa na mahusiano mazuri na Indonesia na kumaliza vita nchini Iraq na Afghaninistan.
0 comments:
Post a Comment