Saturday, 23 January 2016

WOTE KULALA MARUFUKU KUTOKA NJE USIKU TUNISIA.


Mwanahabari kazini.

Tunisia imetangaza amri ya kutotoka nje usiku nchini kote, kufuatia maandamano yenye ghasia kupinga ukosefu wa ajira. Amri hiyo imeanza kutekelezwa saa mbili usiku wa kuamkia leo, hadi saa kumi na moja alfajir. 
 
Wizara ya mambo ya ndani imesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya watu kuharibu mali ya umma na ya watu binafsi katika maandamano hayo yaliyoanza mwanzoni mwa wiki hii na kusambaa nchi nzima. 
 
Rais wa nchi hiyo Beji Caid Essebs amesema Tunisia inakabiliwa na nguvu za nje zinazoutumia mkono wenye dhamira mbaya dhidi ya usalama na utengamano wa taifa. Maandamano yalianzia katika mkoa wa kati wa Kasserine, na kuenea haraka katika maeneo mengine ya nchi, ukiwemo mji mkuu, Tunis.
 
 Takwimu zinaonyesha kuwa ukosefu wa ajira nchini Tunisia umepanda kutoka asilimia 12 mwaka 2010 hadi asilimia 15 mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment

 

COPYRIGHT © Jicho Duniani DESIGN BY DISMAS TEN 0713216125