Bendera ya Bukina faso. |
Burkina faso inandelea na maombolezi ya siku tatu yalioanza jana Jumapili, kuwakumbuka wahanga wa shambulizi la kigaidi usiku wa Ijumaa iliopita..
Burkina Faso na Mali wakati huo huo zimekubaliana kufanyakazi kwa pamoja kupambana na kitisho kinachoongezeka cha wanamgambo wa kundi la Dola la Kiislamu katika mataifa ya Afrika magharibi kwa kubadilishana taarifa za kijasusi na kufanya doria ya pamoja ya kiusalama kufuatia mashambulizi mawili yaliyopangwa katika eneo hilo.
Mawaziri wakuu wa nchi hizo mbili walikutana jana , siku mbili baada ya shambulio dhidi ya hoteli ya Splendid katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.
Rais Roch (ROK) Marc Kabore ameyaeleza mashambulio hayo kuwa ni ya kinyama na ni juhudi za kuidhoofisha nchi hiyo.
Maafisa wamesema wako katika hatua za kuwatambua wahanga waliobaki, ambapo hatua hizo zinakwenda taratibu kutokana na idadi ya juu ya vifo.
0 comments:
Post a Comment